Kituo cha mafunzo cha Benki ya Exim chatunukiwa cheti cha kimataifa cha ubora


PIX 1

Mwakilishi wa Kampuni ya ukaguzi ya ACM Tanzania Tawanda Manyuchi (kushoto) akipeana mkono na Meneja Mwandamizi wa Benki ya Exim – Mafunzo na Maendeleo Priti Punatar kabla ya kukabidhi cheti cha kimataifa cha ubora wa viwango cha ISO kwa kituo cha mafunzo cha benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Akishuhudia wapili kushoto ni Meneja Msaidizi Mafunzo na Maendeleo Japhet Kemboi. (Picha na mpiga picha wetu).

PIX 2

Afisa Fedha Mkuu wa Benki ya Exim Selemani Amani (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa hafla ya kupokea cheti cha kimataifa cha ubora wa viwango cha ISO kilichotunukiwa kwa kituo cha mafunzo cha benki hiyo. Kutoka kushoto ni Meneja Msaidizi Mafunzo na Maendeleo Japhet Kemboi na Mkuu wa kitengo cha kudhibiti Majanga wa Benki ya Exim David Lusala. 

PIX 3

Afisa Fedha Mkuu wa Benki ya Exim Selemani Amani (katikati) akionyesha moja ya machapisho ya mawasiliano ya benki hiyo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa hafla ya kupokea cheti cha kimataifa cha ubora wa viwango cha ISO kilichotunukiwa kwa kituo cha mafunzo cha benki hiyo. Wakishuhudia ni Meneja Msaidizi Mafunzo na Maendeleo Japhet Kemboi (kushoto) na Mkuu wa kitengo cha kudhibiti Majanga wa Benki ya Exim David Lusala (kulia). 

PIX 4

Mwakilishi wa Kampuni ya ukaguzi ya ACM Tanzania Tawanda Manyuchi (kushoto) akiteta na waandishi na wafanyakazi wa Benki ya Exim kabla ya kukabidhi cheti cha kimataifa cha ubora wa viwango cha ISO kwa kituo cha mafunzo cha benki hiyo. Akishuhudia wapili kushoto ni Mkuu wa kitengo cha kudhibiti Majanga wa Benki ya Exim David Lusala. 

Na Mwandishi Wetu

KITUO cha mafunzo cha Benki ya Exim ya Tanzania maarufu kama  ‘Exim Academy’ kimetunukiwa cheti cha kimataifa cha ubora wa viwango (ISO 9001:2008) ikiashiria ubora wa mafunzo yatolewayo na kituo hicho.

Kituo hicho kilizinduliwa na benki hiyo mwaka jana kwa lengo la kuongeza ufanisi na uwezo kwa wafanyakazi na tayari kinatoa programu muhimu za kibenki kwa wafanyakazi wa benki hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kupokea cheti hicho jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Afisa Fedha Mkuu wa benki hiyo, Bw. Selemani Amani alisema cheti hicho kitakua chachu ya ubora na ufanisi wa huduma zilotololewazo na benki hiyo.

“Tunayofuraha kupata utambulisho huu wa kimataifa. Sasa tumeanza kuona kuwa jitihada za benki yetu za kutoa huduma zinazotambulika kimataifa na zenye viwango vya kukidhi matakwa ya wateja wetu ” alisema.

Alisisitiza kuwa cheti hicho kimepatikana kwa muda muafaka hasa benki hiyo ikiwa kwenye utekelezaji wa mpangop kabambe wa uboreshaji kazi na utoaji huduma kwa wateja kwa ujumla.

“Mkakati uliouanzisha na benki yetu miaka michache iliyopita sasa umeanza kuzaa matunda baada ya benki yetu kuibuka mshindi wa jumla katika kipengele cha huduma kwa wateja mwaka jana kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na kampuni ya ukaguzi wa hesabu ya kimataifa ya KPMG iliyotafiti benki 32 nchini Tanzania.

“Mafanikio yasingepatikana bila utendaji mzuri wa wafanyakazi wetu kwa ujumla. Hatutabweteka na mafanikio hayo. Tutaendelea kuwekeza katika utoaji huduma bora kwa wateja wetu vizuri zaidi siku za usoni, ” aliongeza.

Naye Mwaklishi wa Kampuni ya ACM Tanzania Tawanda Manyuchi, kampuni ya kitanzania iliyopewa dhamana na kampuni ya kimataifa ya Uingereza ijulikanayo kama United Kingdom Accreditation Service (UKA) kufanya tathmini ya mifumo ya uongozi wa chuo hicho cha mafunzo cha benki hiyo wakati wa hafla hiyo alisema cheti hicho ni cha kwanza kutolewa kwa chou cha mafunzo kwenye taasisi za kifedha, si kwa Tanzania pekee bali pia na Afrika Mashariki kwa ujumla.

“Kufikia viwango hivyo vya kimataifa inahitaji jitihada nyingi. Ni matumaini yangu kuwa baada ya Benki ya Exim kupata cheti hiki sasa itawekeza nguvu zake kupata viwango vya kimataifa kwenye idara zake zote,” Manyuchi aliongeza.

Leave a comment